Nelly Kazikazi - Interview with City FM
Nelly Kazikazi - Miss Higher Learning 2017/2018
Miss Higher Learning ni mashindano yanayohusisha warembo kutoka vyuo mbalimbali hapa Tanzania. Namshukuru Mwenyezi Mungu, ndugu jamaa na marafiki, waandaaji wa miss higher learning, chuo changu cha IFM na kila mtu aliyeweza kunisaidia kunishinda taji hili. "Naahidi nitawakilisha vizuri wanavyuo wote katika mashindano yanayofuata".
Nelly Kazikazi - CampusLane brand ambassador
CampusLane ni kampuni inayojishughulisha na kuwaunganisha wanachuo wote kutoka vyuo mbalimbali hapa Tanzania kupitia website yao ya www.campuslane.co.tz ambapo km mwanafunzi ukiacha kujuana na kuleta muungano mzuri wa vyuo mbalimbali lakin pia anaweza kujifunza mambo mbalimbali kupitia mtandao huo km vile mambo yanayohusu afya, kujitambua, michezo & burudani, fashion & styles, biashara nk. "Nashukuru uongozi wote wa CampusLane kwa kuniamini na kunipa jukumu hili la kuwa balozi wa CampusLane".
Nelly Kazikazi atembelea Mikumi Nationa Park
Mikumi ni moja kati ya vivutio vizuri vilivyopo Tanzania. Nawakaribisha wageni wote na wazawa kutembelea katika mbuga hii ya wanyama ambayo ina vivutio vingi ukilinganisha na mbuga nyingine. Ukiwa mikumi unaweza kuona wanyama wengi kwa urahisi kama vile Simba, Tembo, Chui, Twiga, Faru na bila kusahau wale simba wanaoweza kupanda juu ya miti, ambao wanaonekana kirahisi ukiwa mikumi ukilinganisha na Serengeti. Mimi kama balozi wa wanachuo na jamii kwaujumla nina wajibu wa kutangaza vivutio vilivyopo katika nchi yangu.
Nelly Kazikazi atembelea kituo cha CHAKUWAMA
Nelly kazikazi Miss IFM 2017/2018 na Miss Higher Learning 2017/2018 nimeweza kutimiza ndoto zangu za kutembelea kituo cha kulea watoto wasio na wazazi CHAKUWAMA na kuwapa msaada kidogo wa baadhi ya mahitaji yao muhimu, "sio kama nimefanya kwaajili ya status bali ni kitu ambacho nilikuwa natamani kufanya kwaajili yangu tu Mimi mwenyewe na najisikia vizuri nimefanikiwa kufanya" nashukuru wote walionisupport mpaka kufikia lengo langu.
Nelly Kazikazi - Miss IFM 2017/2018
IFM ni moja kati ya vyuo vinavyosifika kuwa na warembo wengi sana. Nikiwa kama mshindi wa miss ifm 2017/2018 najisikia furaha kubwa kupata taji hili. "Naahidi kuwa balozi mzuri wa chuo changu na kukiwakilisha vizuri chuo changu". Nashukuru uongozi wa serikali ya wanafunzi IFMSO, wanafunzi wenzangu, waandaji wa shindano hili, ndugu, jamaa na marafiki, walimu na uongozi wote wa chuo.